Burudani ya Michezo Live

Video: Mfahamu Mcongo Alicios Theluji aishiye Kenya, aliyeimba ‘Mpita Njia’ na Juliana wa UG (Interview)

Afrika Mashariki na kati ina kila sababu za kujivunia kuwa na wasanii wanaotuwakilisha vizuri katika ulimwengu wa muziki kwa sasa, na mmoja wao ni mrembo wa kiafrika aitwaye Alicios Theluji.

Alicious-8

Just in-case hujawahi kumsikia au kukutana na hit single yake ‘Mpita Njia’ aliyomshirikisha Juliana ambayo ndiyo kama kitambulisho chake kikubwa katika muziki, basi hii ni fursa ya kumtambulisha kwako, japo naamini tayari ameanza kupata mashabiki wengi Tanzania.

jina lake halisi ni Alice Zeluji Niyonsaba aliyezaliwa mashariki wa DRC (November 1987).

Makazi ya Alicios kwasasa ni Nairobi/Kenya pamoja na Stockholm/Sweden, ambako anachukua masomo ya Business Administration katika chuo cha BTH University.

aa

Alicios anauwezo wa kuimba katika lugha nne, ambazo ni lugha ya nyumbani kwao Kilingala, Kiswahili, Kiingereza pamoja na Kifaransa kwa kutumia style tofauti, kitu kinachochangia kumuongezea mashabiki pande tofauti za dunia.

Alicios ni nani haswa?

“Alicious she is a very very very proud African Girl, She is very humble, she is very hard working, she is a big dreamer, she is very shy, and she is a musician. She is a daughter she is a sister, she is a student”.

Alicios alizaliwa Kivu, Mashariki mwa Congo sehemu ambapo Kiswahili kinazungumzwa. Familia yake ilihamia Kinshasa alipokuwa na miaka mitatu na baada ya kuhamia Kinshasa mama yake alianza kuimba, na Alicios anasema mama yake alikuwa na ndoto za kuwa Mbilia Bell mwingine. Lakini haikuwa rahisi kwake kwasababu alikuwa single mom, ikambidi aachane na muziki.

Alicious16

Jinsi jina la Alicios lilivyopatikana

Kuna siku moja alikuwa na performance (mama yake) yeye na kinadada wengine wa kundi lake na wakaamua kwenda na watoto wao hivyo niliperform nae, na akaniambia nilikuwa naact kama diva na akaanza kuniita Alicios badala ya Alice.
Ni kitu cha kawaida kwa Kinshasa kuwa na nickname au jina la jukwaani kwasababu wale ambao hawawezi kucheza wanaweza kuimba, wale ambao hawawezi kuimba wanaweza kucheza gitaa, so unapata kila mtu ako na nickname, watu wengine wako ka Fally Ipupa ako na nickname ka kumi ama kumi na mbili, so mine was Alicios.

Alicious10

Jinsi alivyoanza kufanya Muziki

Jinsi nilivyoanza kufanya muziki kiukweli siwezi kukumbuka, unajua Kinshasa muziki uko kila sehemu, ni kama life style, kama nilivyosema wale ambao hawawezi kucheza wanaweza kuimba, wale ambao hawawezi kuimba wanaweza kucheza kifaa cha muziki. So unaweza kukuta hata mtoto wa miaka mitatu akiimba wimbo wa Rhumba wa dakika kumi na mbili, kwahiyo nadhani nilianza kupenda muziki bila kujua. Na nilianza kuimba muda mrefu sana uliopita lakini professionally ndio kwanza nimeanza, ‘Mpita Njia’ ndio ilikuwa single yangu ya kwanza.

Alicious5

Kuhamia Kenya

Tulihamia Kenya kama wakimbizi nikiwa na miaka nane, wakati huo sikujua kama ningekuja kuwa mwanamuziki siku moja.
Nachojua napenda muziki napenda kuimba, mfano pale St. Marys mimi ndio nilikuwa naenda kwenye music classes mimi mwenyewe, halafu nilikuwa nikiimba kanisani, nilijua kuwa napenda kuimba lakini sikuwahi kufikiria kwamba nitakuja kuwa mwanamuziki kwasababu mimi ni mtu mwenye aibu sana, halafu mimi ni msomi (kicheko), kwahiyo sio kwamba nilikuwa najua kutoka kitambo, sijui nini kilitokea. Napenda muziki sana lakini ni kitu nimekuwa nikipigana nacho kwasababu ya music industry, na nimekua nikipigana na mapenzi yangu na muziki kwa muda mrefu, lakini ilifika mahali sikuweza kuendelea kupigana nayo tena ndio nikaamua tu wacha nitoe wimbo, hapo ndio nilipoamua kurudi Kenya, na nikafanya album na nikatoa wimbo mmoja kwenye album lakini album hiyo haijatoka hiyo.”

Alicious17


Kuhusu elimu yake

Mi ni msomi, mi ni wale students ka hajapata A hajatosheka, coz unajua tulipohamia Kenya mara ya kwanza nilienda katika shule ya wakimbizi Kabiria….then vile nilienda secondary school nikapelekwa St. Marys…, na sikuwa najua English, but still nilikuwa napata alama nzuri sana and was unbelievable huyu msichana hawezi kuongea Englisha na anapata B (kicheko), how is that possible, so napenda kusoma sana, napenda kupata A inanifanya nijisikie vizuri, ndio maana nilikuwaga nawaza labda nitumie akili yangu ili nije niwe mtu mwingine kama mwanasheria or something. Lakini sasa nafanya muziki, nasoma niko chuo nafanya Marketing, na ninatumaini nitaweza kutumia ujuzi huo katika kazi yangu ya muziki.

Kwasasa ninasoma online, ninaweza kuwa hapa lakini ninasoma Sweden, lakini miaka miwili ya mwanzo ilibidi niwe kule, ilibidi nisomee kule, so nakuja hapa nafanya muziki lakini kila mara inanibidi niende kule kufanya mitihani…Nafanya nachopenda kufanya na nachotakiwa kufanya unajua shule ni kitu ambacho huwezi hepa. It’s a must nafeel good kwasababu ile system nasoma inani allow kufanya music at the same time. “

Alicious7-na mohombi
Alicios na Mohombi

Maisha yake ya Sweden

Nilipohamia Sweden nilikuwa katika kijiji kimoja kidogo kinaitwa Satad, na hapakuwa na watu weusi, na watu ni wakimya sana they are not as social and makelele as we are. So nilitaka kutengeneza marafiki na nilikuwa natakiwa kukaa nyumbani muda mrefu kabla ya kuanza shule. Kwahiyo niliamua kwenda kwenye shule ya muziki kutengeneza marafiki na nikajikuta nimeishia kuimba katika bendi ya Rock (kicheko), hicho ndio nilichofanya. Nilikuwa kwenye Rock band kwa mwaka mmoja, all that in the name of making friends (kicheko). Nilikuwa nikiimba, tulikuwa waimbaji wawili na bendi, tulifanya covers na wakati mwingine tuliandika nyimbo zetu wenyewe, it was very fun, huwezi kujua labda nitakuja kutoa wimbo wa rock wa Kiswahili siku moja, nadhani nahitaji kutumia hizo skills siku moja.

Alicious14

Je anampango wa kufocus kwenye muziki mbeleni?

Yes Definitely, the thing is, siku ina saa 24, una saa 8 za kupumzika kulala, saa nane za kusoma, na saa nane za kufanya kitu unachokipenda kama kucheza mpira au kuwatch movie. And for me music is always fun, sijiskii kama ninafanya kazi napofanya muziki, kulipwa kutokana na kuimba kunanifanya nijihisi…sijui tu siwezi kuelezea. So nina muda wa kutosha nadhani mbeleni ndio nitaendelea kuimba na nitamaliza shule halafu nitafanya vitu vingine sababu unajua maisha ni marefu (kicheko), kuna mengi mtu anayoweza kufanya kama tu akili yako utaielekeza katika kitu hicho.

Alicious12

Akizungumzia album yake ya kwanza Alicios amesema aliandika na kurekodi nyimbo zote kwa siku kumi na nne tu, na ilikuwa na nyimbo nane. Maproducer aliofanya nao kazi katika kuiandaa album hiyo ni pamoja na R-Kay, Musyoka na Dr Eddy.

Alicious14-Juliana
Alicios na Juliana Kanyomozi


Jinsi Alicios alivyoweza kumshirikisha Juliana katika hit yake ‘Mpita Njia’

The collabo with Juliana was a dream come true, ni kati ya vile vitu ambavyo unapanga, lakini unakuwa huna uhakika kama vitatokea lakini unaendelea tu. Nilichokifanya nilienda kwa R-Kay nilimuuliza kama naweza fanya wimbo na Juliana, akaniambia yuko busy sana lakini ukiandika wimbo mzuri kwa Kiswahili hawezi kataa, sababu anapenda kuimba Kiswahili, hawezi kuongea Kiswahili lakini anaimba vizuri. So nilichofanya nilienda home nikaandika wimbo nikaletea R-Kay akaniambia this song is, ah ah si poa nenda kaandike wimbo mwingine najua unaweza kuwa mzuri zaidi, hapo ndio nikaenda home niaandika ‘Mpita njia’, nikaenda nikamuimbia akasema its perfect tukarekodi demo, tukatumia Juliana, kusema kweli sikuwa najua kama atakubali, but akakubali and then akakuja Nairobi tukarekodi, and then nikaenda UG tukafanya video, halafu ika hit.

And now am really really really happy Im very proud of that song I love it so much kwa sababu ni wimbo ambao mama yangu anaweza kuwaonesha marafiki zake bila kuhisi kuaibishwa, am very proud of that song.

Alicious1

Kuhusu style yake ya nywele fupi

Nilirudi Kivu nilipozaliwa kusalimia binamu zangu, and the thing is wao wanalazimishwa kukata nywele zao shule, so walikuwa wanatamani kuwa na nywele refu kama mimi, ndo nikaamua next time nikirudi huko nitakata nywele ndo wafikiri ka short hair is cool. Halafu nikakata nywele. Actually nilikuwa na wig kwaajili ya Mpita Njia video, halafu nikaenda huko vile nitoke huko nikaenda UG kushoot Mpita Njia, Nakumbuka nilikuwa nimekaa na Juliana and we were discussing nivae wig au nikae na kiparaa coz I thought like the kiparaa reminded me of the old me because venye nilikuwa naishi huko hata mi sikuwa na nywele, so there was something about that short hair, so nikaamua niendelee kuwa nazo.

Alicious6-BBC nairobi

Like mother like daughter, Kati ya wanamuziki wote Alicios anampenda sana Mbilia Bell kama ilivyokuwa kwa mama yake.

Baadhi ya single zake zilizotoka ni pamoja na Mpita Njia , Niko Poa na Posa Ya Bolingo.

Katika album yake ya kwanza amewashirikisha wasanii mbalimbali akiwemo Kidumu (Burundi), Juliana Kanyomozi (Uganda), Collo (Kenya) pamoja na wengine.

Ujumbe wa Alicious kwa wasanii wa Kiafrika waishio nje
As an African artist, the more African your music is the better. Let’s Africanise this planet. Let’s do ”us”. Also listen to the music our great grandparents listened too, see if you can modernise it a little bit without totally losing it.

Tazama hapa Interview ya Alicios Theluji na 98 Degrees

SOURCE: ALICIOUSTHELUJI.COM / TAP MAGAZINE

Related Articles

Back to top button
Close
Bongo5

FREE
VIEW