Video: Mfungwa mtukutu duniani aliyetoroka na helkopta gerezani anaswa tena
Baada ya kuchukua miezi mitatu toka kutoroka kwake gerezani hatimae Polisi nchini Ufaransa leo siku ya Jumatano wamefanikiwa kumkamata jambazi sugu, Redoine Faid sambamba na kaka zake wawili huko kusini mwa jiji la Paris.
Chanzo kimoja cha karibu kimethibitisha, Faid ambaye anatokea kwenye kundi la watukutu zaidi nchini Ufaransa lijulikanalo kama ‘notorious ganster’ kuwa amekamatwa.
Jambazi sugu, Redoine Faid
Redoine Faid mwenye umri wa miaka 46 amewahi kutoroka jela kupitia helkopta, kijana huyo mtukutu Julai 1 mwaka huu amewahi kutoroka mbele ya jeshi zito kwakutumia mabomu yanayotoa moshi na kufanikiwa kuvunja dirisha la jela.
Video ikionyesha helkopta aliyotumia kutorokea gerezani
Alitoroka jela alipokuwa anatumikia kifungo chake, baada ya watu wenye silaha nzito kuvamia jela hiyo iliyoko Kaskazini mwa jiji la Paris. Watu hao walimchukua na kuondoka naye kwa kutumia helkopta ambayo walikuwa wameiteka.
Hata hivyo nimarakadhaa kwa Mr Faid kufanya mchezo wake wa kutoroka jela mbele ya ulinzi mkali ambapo mapema leo polisi wamethibitisha pia kukamatwa kwake.