Habari

Video: Mh. Ridhiwani Kikwete azushiwa mazito

Mbunge wa Jimbo la Chalinze, Ridhiwani Kikwete amekanusha kuikosoa CCM kupitia mtandao wake wa Instagram amesema kuwa Account yake ilidukuliwa lakini sasa amefanikiwa kuirejesha mikononi mwake. Tazama video hii akitoa kanusho la taarifa hiyo;

Ridhwani aliandika kupitia mitandao yake ya kijamii kuwa;

Nimesikitishwa sana na hili jambo lililotokea leo.

Watu wameingilia Ukurasa wangu wa Instagram na kunizuia nisiingie kwenye account yangu. Lakini jambo baya zaidi wanalolifanya ni kuandika vitu au maneno ambayo hata sijawahi na sitamani kuyasema.

Nimeshangazwa sana na hili na sijui Nia ya kufanya hivyo ni nini? Malengo yenu hamtafanikiwa.

Mimi niko katika vikao vya halamashauri kupanga bajeti za Halmashauri yetu ya Chalinze.

Hayo maneno na matukio hata hayajawahi tokea.

aliandika Ridhiwani.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents