Habari

Video: Mjadala wa baadhi ya wanaume kuvaa nguo za kike waibuka Bungeni

Naibu Waziri, Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni amesema kuwa hakuna tafsiri ya mavazi ya kike au kiume kwa kuwa mavazi hayo kama suruali yanavaliwa na watu wote wanaume hata wanawake.

Masauni ametoa ufafanuzi huo, leo bungeni wakati akijibu swali Halima Ally Mohamed, Mbunge wa Viti Maalum alietaka kujua serikali inachukua hatua gani kwa baadhi ya wanaume ambao wamekuwa wakijipamba na kujilemba kwa kuvaa nguo za kike.

“Ni kweli kuna wanaume wanavaa mavazi ya kike, hata wanawake pia wapo wanavaa mavazi ya kiume, suala la mavazi lina tafsiri pana, ila sidhani suala la mavazi kama lina tafsiri kuwa vazi hili ni la kike tu na hili ni la kiume tu, nadhani suala hili la Mbunge linahitaji ufafanuzi wake wa kina ili tujue yeye alikuwa anamaanisha nini zaidi katika jambo hili, kwahiyo swali hili limekosa ufafanuzi ndiyo maana nakosa jibu la moja kwa moja” alisema Masauni.

Video:Tazama Serikali ikitoa majibu ya wanaume kuvaa mavazi ya kike na wanawake wa Kiislam kudai kuvulia Hijab na Nikab:

Na Emmy Mwaipopo

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents