Aisee DSTV!

Video: Mkubwa Fella afunguka kuhusu Rich Mavoko na Wasafi Festival ‘Nampigia debe mwanangu Juma Nature naye awepo’

Meneja wa msanii wa muziki wa Bongo Fleva, Diamond Platnumz, Mkubwa Fella amesema kuwa milango ipo wazi kwa Rich Mavoko kushiriki tamasha la Wasafi Festival.

Katika mahojiano yake na Bongo5 Alhamisi hii, Fella amesema kuwa ndiyo sababu wakasema hii ni yawatu wote hivyo hawana mapingamizi na mtu ilimradi tu akikubaliana na alichopewa.

‘Tumesema hii ni ya kwetu sote, hatuna mapingamizi na mtu fulani akikubali pakeji aliyogewa na yeye akakubali kufanya basi anaruhusiwa mtu yoyote,” amesema Fella.

Mkubwa Fella ameongeza ”Mimi mwenyewe nampigia debe mwanangu Juma Kasimu Ally Kiroboto naye awepo, kuna watu wengine zamani walikuwa wanafikiria Fella yuke vile kumbe hayupo hivyo wao walibebeshwa upumbavu na watu wengine.”

”Lakini Juma Nature hayuko vile na mimi siko hivyo, sisi tunaelewana sana lakini kunawatu walipandikiza chokochoko.”

Related Articles

Back to top button
Bongo5

FREE
VIEW