Habari

VIDEO: Mkulima kutoka Bukoba ajishindia Tsh mil. 10 kupitia droo ya ‘Shinda na M-PAWA’ kutoka @VodacomTanzania

Kampuni ya simu za mkononi ya Vodacom Tanzania kushirikiana na Benki ya CBA wamemtangaza  mshindi mkuu wa kampeni ya ‘‘SHINDA NA M-PAWA’’ iliyofikia tamati leo Desemba 13, 2018. Mshindi huyo aliyejinyakulia kitita cha milioni kumi ni Sophia Sarapion kutoka Bukoba.

Mkurugenzi Idara Usajili wa hazina wa Benki ya Biashara Afrika CBA Hakim Sheikh (kulia) akipiga simu kwa mmoja wa washindi wakati wa droo ya mwisho ya Promosheni iliyokuwa inakwenda kwa jina la Shinda na M-PAWA. kushoto ni Meneja Masoko wa Vodacom, Noel Mazoya, pamoja na Mkaguzi wa Bodi ya Michezo ya Kubahatisha ,Abdallah Hemedy.

Washindi wengine watano waliopatikana kwenye droo hiyo kubwa wamejinyakulia bajaji moja moja ni Abeid Abeid, Lucas Ngoye, Mariamu Barawa, Hassan Msabila na Hamisi Mpela.

Promosheni hii iliyowalenga, wateja wote wa M-PAWA nchini, imetengenezwa kwa ajili ya kuwasaidia watumiaji wa Vodacom kujiwezesha kifedha ili waweze kujiwekea utaratibu wa kuweka akiba na kuwahimiza kurudisha mikopo mapema kwa riba za chini kabisa kwa muda wa wiki 6 kuanzia tarehe 8 Novemba 2018 kukiwa na jumla ya wateja 1,296 wanaoshinda kwenye droo za kila wiki. Sambamba na draw ya washindi wa mwisho droo hiyo imemalizia idadi ya wateja 200 waliongeza mara mbili ya amana na wateja 15 walioweza kuchukua na kurejesha mikopo yao kabla ya wakati.

Wakizungumza kwenye muendelezo huo, washindi walitoa shukrani zao kwa Vodacom na kuwapa fursa hiyo ya kuwatuza na kuwawezesha wateja kupitia kampeni ya “SHINDA NA M-PAWA’’.

Katika maneno yake, Meneja Masoko wa kitengo cha M-PESA kutoka Vodacom, Bw. Noel Mazoya, aliipongeza Benki ya CBA kwa kuendesha promosheni hiyo kwa uadilifu na uwazi.

Alithibitisha kuwa zoezi la kuchagua washindi hao lilifuata utaratibu toka mwanzo wa kampeni Novemba 2018 hadi kuibuka kwa washindi mbalimbali. Aliwahimiza wateja wenye bahati, hasa wale washindi, kutumia zawadi zao vizuri, na kusisitiza, ” ni muhimu kuwekeza kwa ufanisi ikiwa ni pamoja na kukupa ushauri bure unapohitaji”.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents