Tupo Nawe

Video: ‘Morrison alikuwa katika klabu ya Mjomba wangu, nilimwambia asimuuze’- Mwinyi Zahera 

Aliyekuwa Kocha wa Klabu ya Mabingwa wa Kihistoria Ligi Kuu soka Tanzania Bara Yanga, Mwinyi Zahera amemzungumzia mchezaji anayekuja kwa kasi na kujizoelea umaarufu ndani ya timu hiyo ya Wananchi, Bernard Morrison.

Zahera amesema Morrison ni mzuri na alitamani sana zama zake alivyokuwa Yanga angekuwa na aina hii ya mchezaji huku akienda mbali zaidi vile anavyomjua

”Morrison nilianza kumjua tangu alivyokuwa Congo, alikuwa Vita Club alianza pale Vita, na Rais wa Vita Club ni Mjomba wangu. Mjomba ndugu yake na mama yangu, hata mimi kuja Congo timu ya Taifa nikitoka Ulaya alinipokea.”- Zahera

Mwinyi Zahera ameongeza kuwa ”Wakati Vita Club wanamuuza Morrison, nchini Afrika Kusini nikamwambia kocha ‘Ibenge’ huyu ndiyo mchezaji ambaye anaweza kubadili matokeo muda wowote uwanjani kwa nini mnamuuza. Rais akasema wa Vita akasema Morrison alikuwa anapenda kwenda Afrika Kusini, nikawaambia mnapoteza kitu kikubwa sana.”

”Mechi nyingi Morrison ndiyo amekuwa akileta mabadiliko, hata kama mechi itakuwa ngumu lakini kwa uwezo wake anabadili matokeo.”

Related Articles

Back to top button
Close
Bongo5

FREE
VIEW