Jiunge ufaidi miezi 2 bure!

Video mpya ya wimbo wa Feza Kessy ‘Amani Ya Moyo’ kutoka leo

Ulikuwa unaisubiri kwa hamu video ya Feza Kessy?, kama umejibu ndio basi hii ni habari njema kwako sababu mwongozaji na mtayarishaji wa video hiyo Nisher amethibitisha kutoka kwa video hiyo leo Jumatatu (June 17).

feza-kessy

By the way sijakuuliza kama unafahamu Feza Kessy ni mwimbaji pia, ndio! namaanisha huyo huyo Feza wa BBA, she is a singer japo jina lake bado halijaweza kushine sana upande huo. Kabla hajaenda BBA aliacha ametoa wimbo wake unaoitwa ‘Amani Ya Moyo’ na pia alikuwa ame shoot video ambayo ilikuwa bado haijatoka.

Kupitia ukurasa wake wa facebook muongozaji na mtayarishaji wa video hiyo Nisher wa Nisher Entertainment, asubuhi ya leo ametoa taarifa kuwa video hiyo inatoka masaa 12 kutoka muda alipoiweka post hiyo 10:22AM leo.

“Masaa 12 Kuanzia sasa Nisher Entertainment itatoa Kazi Mpya Ya Mwana Dada Feza Kessy (BBA2013) …. ni video yake aliyoifanya na Mtu wako wa Nguvu….. Je unajua Ni wimbo gani nauongelea?? Kama hujui Tupia macho Youtube Baada ya masaa 12….. #TEAM BYBEE ARE YOU READY??????? I CANT HEAR YOU……”

Audio ya wimbo huo ilitoka (February 11) mwaka huu.

Related Articles

Bongo5

FREE
VIEW