Jiunge ufaidi miezi 2 bure!

Video: Mtangazaji aripoti kifo cha mumewe aliyepata ajali live

Supreet Kaur alikuwa akisoma habari kupitia kituo cha runinga cha IBC24 huko India Jumamosi iliyopita na akapata breaking news kuwa kuna ajali mbaya ya gari imetokea.

Aliwaambia watazamaji kuhusu kilichotokea – watu watatu wamepoteza maisha na wengine wawili kujeruhiwa baada ya gari ya SUV kugongana na roli huko Pithora.

Wakati akimsikiliza ripota akitoa taarifa za ajali hiyo kwenye simu, Kaur alianza kuhisi kuwa mume wake aliyekuwa maeneo yale yale na gari kama hiyo huenda akawa mmoja wa waliopata ajali.

Lakini alijikaza na kuendelea kuripoti licha ya picha zilizofifishwa kuoneshwa pamoja na gari yenyewe.

“She was doing her job, and she kept on doing it with composure and without showing her emotions on air,” IBC24 alisema mhariri mkuu wa kituo hicho, Ravi Kant Mittal.

Kaur alianguka kilio kuomboleza kifo cha mumewe baada ya taarifa kuisha. Kaur na mumewe Harshad Kawade walikuwa wameona kwa miezi 18.

Related Articles

Bongo5

FREE
VIEW