Burudani

Video: Mtazame Shetta akiongelea video ya ‘Shikorobo’

Jumatano hii Shetta ataachia video ya wimbo wake ‘Shikorobo’ aliomshirikisha msanii wa Nigeria, KCEE.

Video ya wimbo huo imefanyika nchini Afrika Kusini.

Akiongea na Bongo5, Shetta amesema kuwa ‘Shikorobo’ ni neno alilolitunga tu na lililomuijia wakati anarekodi wimbo huo.

“Shikorobo nimeiletea maana yake kwamba umenimaliza au unaweza kusema you kill me kwa kitu ambacho unakifanya, kitu ambacho ni kizuri zaidi,” amesema.

Rapper huyo amedai kuwa wimbo huo ni wapenzi lakini ameufanya uwe wa kuchezeka zaidi.

Amedai kuwa aliamua kumpa kazi kwa mara nyingine tena Godfather kutengeneza video yake kwa kuwa ni muongozaji anayemjali msanii na hupenda kumsikiliza mteja wake kile anachokitaka na sio kulazimisha mawazo yake.

Kwa upande wa gharama alizotumia kukamilisha video hiyo, Shetta amesema hatopenda kuzitaja bali ubora wa video ndio utajieleza wenyewe.

Mtazame zaidi hapo juu.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents