Burudani

Video: Muhitimu wa ‘Computer engineering and Information Technology’ akutana na haya alipotangaza kujiunga na uigizaji

Baada ya kampuni ya DStv Tanzania kuwapata washindi wanne kwenye shindano lao la MultiChoice Talent Factory watakao kwenda Nairobi, Kenya kwenye kambi maalumu ya kujifunza kuandaa filamu mmoja wa washindi hao, Sarah Kimaro ambaye anaujuzi wa Computer engineering and Information Technology kutoka chuo kikuu cha Dar es salaam ameelezea changamoto aliyokumbana nayo kutoka kwa wazazi wake alipotangaza kuhitaji kuhamia upande wa pili wa sanaa ya maigizo na kuachana na taaluma yake.

”Nimemaliza chuo kikuu cha Dar es salaam mwaka jana kozi ya Computer engineering and Information Technology baada ya kumaliza chuo kuna nafasi nyingi zilikuja za kufanya kazi lakini sikuvutiwa nazo wazazi wakawa wananiuliza unafanya nini mjini kila siku wananiuliza unafanya nini mjini.”

”Kuna wakati nilijiunga na kampuni ya msanii wa filamu Dk. Cheni nikawa nafanya kazi ya ‘production’ ni kawaambia wazazi hawakunielewa ikawa kama kuna ugomvi na mama angu akiniambia nikafanye kazi kwenye kampuni ambazo nimechaguliwa ikawa kuna matatizo mengi lakini mimi siku sita nikaendelea na kazi yangu nilipoona ugomvi un azidi ni kabidi niende kuajiriwa na kampuni yenye kazi za taaluma yangu.”

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents