Michezo

Video: Mwamuzi achezea kichapo cha ‘mbwa koko’ ligi kuu Ethiopia

Mchezo wa soka unafahamika zaidi kwa kuwaunganisha watu pamoja na kuleta amani, lakini kwa baadhi ya timu zimekuwa zikiufanya mchezo huo kuonekana kama ni vita.

Hasa kitendo cha kuwapiga waamuzi kimekuwa kikisamiri kila kukicha japo adhabu kali zimekuwa zikitolewa kwa vilabu vinavyofanya matukio hayo. Tukio jingine kama hilo limetokea katika ligi kuu ya Ethiopia Jumapili iliyopita.

Katika mchezo huo ambao ulichezwa kwenye uwanja wa Addis Ababa, uliwakutanisha timu ya jeshi ya Defence Force na ile ya chuo kikuu nchini humo Welwalo Adigrat University, ilishindwa kumalizika kutokana na vurugu za kupigwa kwa muamuzi wa mchezo huo.

Wachezaji wa Welwalo Adigrat na viongozi wa benchi la ufundi walimvamia na kumpiga mwamuzi kwa madai ya kulikubali goli la wapinzani wao ambalo mpira haukuvuka mstari wa goli.

Mpaka mchezo huo unavunjia timu hizo zilikuwa zimefungana bao 1-1. Wakati huo huo ligi hiyo kwa sasa imesimama kutokana na tukio hilo lisilokuwa la kimchezo.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents