Moto Hauzimwi
TECNO Spark 2

Video: Nampenda sana Shamsa Ford na Wema Sepetu – P The Mc

Rapper wa SSK, P The Mc amesema miongoni mwa mastaa wote wa kike Bongo aliowataja katika ngoma yake mpya ‘Mademu Wangu’ anavutiwa zaidi na Shamsa Ford na Wema Sepetu.

Katika ngoma hiyo verse ya kwanza amewataja Aunt Ezekiel, Linah, Jokate, Wolper na na Shamsa Ford na verse ya pili amewataja Shilole, Wema Sepetu, Kajala, Hamissa Mobetto na Snura ambapo ametaja yupi anamvutia kwenye kila verse.

Shamsa Ford nampenda sana si kwamba sababu ya uzuri nampenda sababu ya tabia, yaani ni tofauti sana na tabia za wasichana wengi ambao tumewazoea kwenye hii industry” P The Mc ameiambia Bongo.

“Hapo mkali Wema Sepetu, hapingi mtu yule ni Tanzania Queen, msichana mmoja mwenye haiba, mwenye nguvu anaweza akaongea kitu wote tukakisikiliza au kukizingatia,” amesema.

P The Mc amefanya refix ya ngoma ya Ngwea ‘Mademu Wangu’ ya kitu ambacho ameeleza kuwa amepewa baraka zote na Bongo Records ambao ndio wenye haki miliki ya ngoma hiyo.

Related Articles

Bongo5

FREE
VIEW