DStv Inogilee!

Video: Nay wa Mitego atua BASATA, afunguka alichoitiwa ikiwa ni siku chache toka aachie wimbo ‘Alisema’

Msanii wa muziki wa Hip Hop Nay wa Mitego Jumanne hii majira ya nchana alitua Baraza la Sanaa Taifa (BASATA) baada ya kupigiwa simu kwamba ana barua yake.

Rapa huyo amedai kwamba alidhani barua hiyo itakuwa inahusu wimbo wake mpya ‘Alisema’ ambao ameuachia siku chache zilizopita.

“Kusema kweli baada ya kupokea simu ya BASATA niliishiwa nguvu kabisa, lakini baada ya kufika eneo la tukio nikakuta ni barua kuifungua kumbe ni ishu za kazi,” alisema Nay wa Mitego.

Aliongeza, “Unajua lazima nishtuke kwa sababu mimi nikiona simu za BASATA lazima akili iwake kidogo, lakini kumbe ni jambo la kawaida na kwa bahati nzuri nilipigiwa simu na mtu mkubwa kutoka BASATA akanisifia. Pia nimepokea simu za wabunge na mawaziri wanaonekana kuukubali wimbo Alisema”

Related Articles

Back to top button
Bongo5

FREE
VIEW