Habari

Video: NEC yatoa taarifa ya upotoshaji wa matokeo ya uchaguzi mdogo wa jimbo la Dimani

Mkurugenzi wa Tume ya Taifa ya uchaguzi (NEC), Ramadhani Kailima ametoa ufafanuzi juu ya taarifa za upotoshaji wa matokeo ya jimbo la Dimani Zanzibar.

Kailima amesema kuwa wapiga kura walioandikishwa katika jimbo la Dimani, Zanzibar ni 9,275.

“Napenda kuwafahamisha wananchi wote kuwa taarifa sahihi za matokeo ya kura katika Uchaguzi mdogo wa Ubunge Jimbo la Dimani ni kama ifuatavyo; Wapiga Kura walioandikishwa jimbo la Dimani ni 9,275, Waliopiga Kura walikuwa 6,406, Kura halali 6,172 na Kura zilizoharibika ni 234,” amesema.

Mtazame wakati akitoa taarifa hiyo:

Uchaguzi huo wa ubunge jimbo la Dimani ulifanyika tarehe 22, Januari 2017.

BY: Emmy Mwaipopo

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents