Burudani

Video: Nelly, mtoto wa Amitabh Bachchan, Abhishek na muimbaji wa Canada, Raghav waachia wimbo wa kampeni ya kuleta umeme wa jua Bongo

Muimbaji nyota wa nchini Canada mwenye asili ya India, Raghav Mathur ameachia wimbo ‘Until the Sun Comes Up’ aliowashirikisha muigizaji wa Hollywood, Abhishek Bachchan na rapper wa Marekani Nelly kama sehemu ya mradi wa kuleta umeme wa jua nchini Tanzania.

Kutokana na mradi huo kupitia taasisi ya SolarAid, Raghav alisambaza taa 300 zinazotumia umeme wa jua kwenye shule ya sekondari ya Shubugubwen ya Mkuranga mkoani Pwani.

Taa hizo zinaonekana kwenye video hiyo pamoja na wanafunzi wa shule hiyo.

Mwanzoni mwa video hiyo rapper Nelly anaonekana akisema ‘It’s your boy Nelly sending a special shout out to my boy Raghav and Solar Aid for holding down Tanzania 300 solar rights.”

Picha za video hiyo zilichukuliwa September mwaka jana.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents