Moto Hauzimwi
TECNO Spark 2

Video: Nemo aelezea alivyopokea mashabiki kufananisha nyimbo zake na Ne-Yo

Nemo amefunguka jinsi alivyokuwa anajiskia wakati mashabiki walipokuwa wanamfananisha na msanii Ne-Yo wa Marekani.

Akiongea na Bongo5, msanii huyo amesema, “Kiukweli niliipokea vizuri sana mimi mwenyewe sikutegemea lakini ilikuwa ni ndoto zangu kwamba nifanye vitu kama wanavyofanya wakina Ne-Yo, lakini baadae ikaja automatic kwa watu wamechukulia hivyo hivyo kama Ne-Yo.”

“Kwa hiyo nikaona lengo iliyokuwa nafikiria ni mule mule, nikaangalia mpaka video nitakavyo act na nitakavyocheza, jinsi nitakavyovaa na jinsi nitakavyoimba na kutumia ule uwezo na hata steji nitakavyokuwa. Kwa hiyo waliwakaona duuh ni kama ni Ne-Yo, nilifurahi sana,” ameongeza.

Msanii huyo alianza kufananishwqa na Ne-Yo mara baada ya kuachia wimbo wake wa ‘I Need Wife’ ambao pia ulimfanya kuteka mashabiki wengi zaidi.

Related Articles

Bongo5

FREE
VIEW