Moto Hauzimwi
TECNO Spark 2

Video: Nemo anayefananishwa na Neyo aeleza sababu ya ukimya wake wa miaka mingi

Je unamkumbuka msanii wa Bongo Flava Nemo ambaye wimbo wake wa ‘I Need Wife’ ulikuwa kama wimbo wa taifa? Basi msanii huyo amefunguka sababu ya ukimya wake wa muda mrefu kwenye tasnia ya muziki na jinsi anavyoona Bongo Flava kw sasa.

Akiongea na Bongo5, msanii huyo amesema, “Kiukweli huu ni muda muafaka wa kuwafahamisha ni sababu gani, nilikuwa busy kidogo na masomo nikakatisha mambo yangu ya muziki kwa sababu ilikuwa Ini vigumu sana kuchanganya muziki na masomo wakati mmoja. Nikaona niegemee kwenye masomo kidogo lakini bado ile hamu ya kufanya muziki ilikuwa bado ipo, kwa hiyo nilikuwa nafanya mazoezi sikukaa kimya tu kama nimekaa. Nimerekodi nyimbop lakini nilikuwa sipo tayari kuachia.”

Nemo ameongea pia kuhusu kimya chake kama kinaweza kikawa kimewapoteza mashabiki wake au ndio kitawavuta mashabiki wengine ambao walikuwa hawamfuatilii.

“Katika research yangu nilivyoona wengine wameoongezeka, wengine wamekuwa kama wanakumbuka walikuwa mashuleni. Ingawaje wengine baadhi niliwapoteza na kuwaudhi wengine kwamba huyu jamaa tulishaanza kupata mzuka naye katutoroka hivyo. Kila sehemu ninapokwenda ilikuwa kama kesi na kila ninapokaa siishiwi kuulizwa,” amesema Nemo.

Msanii huyo ameongeza jinsi anavyouona muziki wa Bongo Flava kwa sasa, “Nimependa sana jinsi muziki unapoenda na uvyoelekea, umepanuka pia na umepanda. Ninaweza nikasema kwamba mimi nilikuwa nafanya vile vitu nilitangulia, yaani inawezekana nilikuwa nafanya vitu ambavyo vilitakiwa nije kuvifanya miaka ya sasa hivi au ya baadae lakini nilianzisha kufanya zile RnB ngumu kali kama za kinyamwezi na ilikuwa ni muda mrefu sana.”

“Lakini kwa sasa hivi naona muziki umekuwa na watu wanafanya na unakubalika muziki, unaenda kimataifa watu wanafanya vizuri na wasanii kadhaa ambao wanachipukia nao wanafanya vizuri na hata wazamani pia waliokuwepo baadhi wanafanya vizuri na wengine wamepotea,” amesisitiza.

Kwa sasa msanii huyo anasimamiwa na uongozi mpya wa kampuni ya Digital City Drimz.

Related Articles

Bongo5

FREE
VIEW