Bongo Movie

Video: Nyumbani kwa Wema tulikuta misokoto ya sigara – Shahidi Kesi ya Wema

Kesi inayomkabili malkia wa filamu Wema Sepetu ya kutumia dawa za kulevya imeendelea kuunguma Jumatatu hii katika mahakama ya Kisutu jijini Dar es salaam ambapo upande wa mashtaka uliendelea kutoa ushahidi kupitia mashahidi wake wawili wa mwisho mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Thomas Simba.

Shahidi wa kwanza Steven Nondo ambaye ni mjumbe wa serikali ya mtaa anaoishi Wema Sepetu, alisema alipigiwa simu na mtu asiyemfahamu akitakiwa kufika nyumbani kwa Wema Sepetu.

Baada ya kufika eneo la tukio, shahidi huyo aliimbia mahakamani kwamba akitakiwa kusimamia kupekuliwa kwa nyumba ya malkia Wema Sepetu ambaye analikuwa anatuhumiwa kutumia dawa za kulevya.

“Tulianza kupekua jikoni katika makabati la vyombo tukakuta msokoto wa sigara, sijui kama ni bangi nachojua kwamba ni msokoto,” alisema Shahidi huyo.

Pia shahidi huyo alisema wakati wanajiandaa kuingia ndani walikaguliwa kwa kusachiwa na mdogo wake Wema Sepetu ili kujiridhisha kama hawana kitu.

Wakili wa utetezi Alberto Msando alimuuliza shahidi huyo kama ni kweli katika chumba cha Wema walikuta kitu chochote na shahidi huyo alijibu kwamba hakukuta kitu chochote kwenye chumba cha Wema Sepetu.

Naye shahidi wa pili katika kesi hiyo ambaye alikuwa mhifadhi vithibiti katika Kituo cha Polisi cha Kati, alikiri kupokea vithibiti hivyo kutoka kwa Afande Willy na yeye kuvipeleka kwa mkemia Mkuu kwaajili ya kufanyiwa vipimo.

Shahidi huyo alidai alipokea vithibiti hivyo vikiwa wazi na yeye alivipokea na kuvihifadhi katika bahasha maalum.

Baada ya kusikiliza ushahidi huo, Hakimu huyo alifunga ushahidi wa upande wa mashtaka na ndipo wakili wa upande wa utetezi, Alberto Msando alipoiomba mahakama kumuachia Wema Sepetu pamoja na washtakiwa wengine wawili kwa kuwa hawana cha kujibu kutokana ushahidi uliotolewa. Kesi hiyo itaendelea kusikilizwa April 3 mwaka huu.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents