Burudani

Video: Ommy Dimpoz akieleza maana ya wimbo wake mpya ‘Tupogo’ aliomshirikisha J.Martins

Hivi karibuni hitmaker wa Me and You, Omar Faraji Nyembo aka Ommy Dimpoz anatarajia kuachia wimbo mpya uitwayo Tupogo aliomshirikisha msanii na producer wa nchini Nigeria, Justice Martins aka J.Martins.

Wimbo huo umetayarishwa kwa ushirikiano wa Marco Chali wa MJ Records na Man Walter wa Combination Sounds. Bongo5 imezungumza na Ommy Dimpoz kutaka kufahamu maana ya jina la wimbo huo.

“Tupogo ni neno la kubuni ambalo nimelibuni mimi mwenyewe kama nilivyobuni Nai Nai,”amesema Ommy.

“Kwahiyo Tupogo ni jina jipya naweza kusema au msemo mpya kabisa mjini ambao ni tupo na tuna go. Kwahiyo unaweza ukawa na maana moja ama mbili tofauti kwa maana kuna kuna ‘tupo’ na ‘tunago’ katika hali ya mapenzi, mtu na mpenzi wake kwa maana labda mengi yashasemwa lakini nyie mtaongea sisi tupo na tutaendelea kuwepo

Nimejaribu kufanya utafiti, unajua wakati mimi mwanzo nilivyoanza kutoa kazi zangu hizi, nilikuwa nimechanganya mahadhi ya West Africa kwa kuchanga na Bongo Flava fulani hivi, mpaka watu wakawa wanatafuta nyimbo za kuonekana kwamba mimi labda nimecopy sehemu. Kwasababu ilikuwa style iliyokuja ghafla halafu ikashika sana. Nilikuwa najaribu kutumia akili ya ziada katika ubunifu wangu.

Ukisikiliza muziki wa Tupogo, nimejaribu kuweka kitu fulani more African, kuna Utanzania, yaani muziki uflani mpya katika industry ya Bongo Flava .

Ommy amesema anatarajia kuuachia wimbo huo katika mwezi huu wa Ramadhan.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents