Michezo

Video: Pangua pangua ya ratiba ya ligi yamponza Wambura

Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini (TFF) likiwa chini ya uongozi mpya wa rais, Wallace Karia limeanza kuchukua hatua kwa bodi ya ligi (TPLB) ambayo inadhamana ya kupanga ratiba ya mashindano yote ya ligi kuu, daraja la kwanza na la pili kwa kitendo cha kupanga ratiba bila ya kuzingatia michezo ya kimataifa hali iliyopelekea kuvurugika mapema.

Akizungumza na waandishi wa habari Kaimu Katibu Mkuu wa TFF, Alfred Kidao amesema Bodi ya ligi imeshindwa kupanga ratiba vizuri hivyo kupelekea kuwepo na viraka mwanzoni kabisa  mwa msimu na hii ni kutotilia maanani kalenda ya FIFA na mambo mengine hivyo kuonekana bado kunachangamoto katika upangwaji wake.

“Nimeagizwa na rais nimwandikie barua mtendaji mkuu wa bodi ya ligi ili aweze kuwachukulia hatua viongozi wa bodi hiyo waliohusika na kupanga ratiba” alisema Kaimu huyo wa TFF, Kidau.

Alfred Kidao ambaye anasiku tisa pekee toka kuteuliwa kwake ameongeza kuwa “Nimewapa kazi ya kuipitia ratiba ya ligi kuu waandamizi watatu kutoka makao makuu ya TFF na Afisa mmoja kutoka Bodi ya Ligi mpaka tarehe mbili waje na ratiba ambayo haitabadilishwa mpaka mwisho wa msimu rabda yatokee mambo ambayo yapo nje ya uwezo wetu ya kibinadam mfano mvua na kadhalika”.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents