Michezo

Video: Picha za Selfie zamponza dereva pikipiki

Dereva wa pikipiki nchini Uingereza, Pawel Zietowski amehukumiwa kifungo cha miezi nane jela baada ya kukutwa na kosa la kuendesha chombo hicho cha moto huku akiwa ameinua tairi moja juu na kujipiga picha za Selfie.

Pawel Zietowski mwenye umri wa miaka 27 mkazi wa Warrington amefanya tukio hilo la kijipiga picha za Selfi wakati akiwa katika spidi 177 kwa saa kabla ya kusimamishwa eneo la Staffordshire tarehe 2 Juni .

Wakati akiendesha pikipiki hiyo alikuwa akichukuliwa na video bila yeyemwenyewe kutambua huku alikuwa akifanya hivyo kwa kuonyesha bodaboda yake mpya aina ya Yamaha R6 bike.

Wakati wa kusomewa kwa hukumu yake, Jaji Judge David Fletcher amesema kuwa picha yake “ilikuwa ya kusisimua na kuogofya”.

Zietowski amekiri kutenda kosa hilo la kuendesha kwa hatari.huku akisema kuwa hupenda sana kushiriki mashindano ya pikipiki na alikuwa akijizoweza bara barani.

Habariza kijana Zietowski zimeenea ghafla katika vyombo mbalimbali vya habari wakati mahakama ikimpiga marufuku kuendesha chombo chochote kile kwa muda wa miaka miwili na miezi minne.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents