Habari

Video queen Vera Sidika wa Kenya apata shavu la kuwa ‘cover model’ wa jarida la ‘King Magazine’ la Marekani

Napomzungumzia Vera Sidika aka Vee S. beiby au kama wakenya wanavyopenda kumuita ‘miss Big booty’ nakuwa namaanisha yule mrembo aliyeipamba video ya P. Unit ‘You Guy’. Uzuri wa mrembo huyo umemfanya aweze kuteka hisia za mashabiki wengi (hususan wanaume) lakini pia unamsaidia kupata michongo mbalimbali hata nje ya nchi yake.

vera 22

Mtandao wa Daily Post wa Kenya umeripoti kuwa Vera amepata dili ya kutokea katika jarida la wanaume ‘King Magazine’ la Marekani kama ‘cover model’ katika toleo lijalo. King Magazine ni jarida la ‘African-American’ kwaajili ya wanaume ambalo huandika habari za watu maarufu, hip hop, fashion, michezo pamoja na warembo wa videos ‘video vexens’.

vera-2

Shavu hili limekuja ikiwa ni siku chache tu toka Vera atokee katika top ten ya video vixens wa Africa iliyotolewa na Channel O akikamata nafasi ya 4.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents