Moto Hauzimwi
TECNO Spark 2

Video: Quick Rock- Hakuna msanii asiye kopi

C.E.O wa Switch Music Group (SMG) Quick Rock ametoa ufafanuzi juu aina ya muziki unaofanywa na kundi la OMG lililopo chini ya lebo yake.

Akiongea na Bongo5, msanii huyo amesema kuwa hakuna msanii anayefanya muziki bila kopi muziki kutoka sehemu nyingine kwani hata yeye kuna watu alikuwa anawasikiliza na kuwafatilia katika muziki.

“Hakuna msanii mwenye style yake kila msanii kuna mtu amemu-inspire mimi sikuanza tu kuchana, nilianza kuimba kwaya kanisani Sunday Schoo lakini mimi kuchana Tang twist wakati nipo sekondari nilikuwa nasikiliza sana nyimbo za Buster Rhymes nilikuwa napenda kumsikiliza sana A.Y nilikuwa napenda kumsikiliza sana marehemu Mangwear na wengineo nilivutiwa sana na aina yao ya muziki,” amesema Quick Rock

Akaongeza “Nawaona mbali sana OMG  kwa sababu there very talented wana displine na wanapenda sana muziki na kitu wanachofanya, nawaona mbali sana kikubwa nacho waambukiza kuwa there is busness in music, unaweza ukawa unapenda sana muziki ukawa attach sana na muziki then ukasahau kuwa muziki ni biashara, so love the music , enjoy the music make music but don’t for get is busness.”

Na Salum Kaorata

Related Articles

Bongo5

FREE
VIEW