Habari

Video: ”Rais Magufuli akalijua hili mapema, Ukipiga chafya ukichekiwa una Corona,”- Polepole

Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Humphrey Polepole amesema hii leo tarehe 22 Mei 2020 kuwa Chama cha Mapinduzi (CCM) kuanzia leo kimeruhusu shughuli zote kuendelea baada ya kufungwa kwa muda ili kuepusha kusambaa kwa virusi vya ugonjwa wa Coroan.

”Chama cha Mapinduzi, baada ya kufuatilia, kutathmini hali na muelekeo wa ugonjwa huu #Corona, tunasema shughuli za Chama cha Mapinduzi zote sasa ruksa. Na tunapoendelea kufanya shughuli za Chama, tuendelea kuzingatia maelekezo ya wataalam na tuzijulishe mamlaka za Chama na mamlaka za kiserikali.”- Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Humphrey Polepole

”Chama cha Mapinduzi kingependa kuwajulisha mpaka sasa, heshima yake katika Dunia na Afrika imeongezeka mara dufu. Chama chetu ni Chama kiongozi hapa Afrika, Chama chetu ni chama kiongozi Kusini mwa Afrika, chama chetu kwa wingi wa wanachama ukilinganisha na idadi ya watu hapa Tanzania, Chama cha Mapinduzi ndiyo chama kikubwa ulimwenguni, ukizungumzia wingi wa wanachama peke yake chama cha kikomonist cha watu wa China kitakuwa ndiyo kikubwa alafu chama cha Mapinduzi kinafuata lakini ukisema wingi wa wanachama kwa uwiano wa idadi ya watu CCM ni chama kikubwa ulimwenguni na hapa Afrika.”- Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Humphrey Polepole

 

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents