Aisee DSTV!

VIDEO: Rais Magufuli akubali ombi la RC Makonda kwenda Misri, Awapongeza Taifa Stars licha ya kupigwa na Senegal “Kufungwa bao mbili, Wamejitahidi”

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe Dkt. John Pombe Magufuli amekubali ombi la Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Mhe. Paul Makonda la kutaka kwenda nchini Misri kuihamasisha timu ya Taifa Stars kwenye michuano ya AFCON 2019 inayoendelea nchini humo.

Rais Magufuli akihutubia Taifa mapema leo asubuhi wakati wa uzinduzi wa ghala la gesi la Kmapuni ya Taifa Gas Ltd. Amesema kuwa lengo la Watanzania kwenye michuano hiyo ni ushindi hivyo kama RC Makonda atakwenda kuongeza hamasa, haina haja ya kumakatalia asiende.

RC Makonda awali alinyimwa ruhusa ya kwenda nchini Misri kwenye mchezo wa kwanza wa Taifa Stars dhidi ya Senegal, Ambao Stars walifugwa goli 2-0.

Kwa upande mwingine, Rais Magufuli ameeleza kufungwa kwa Stars kuwa ni hali ya mchezo na ni kawaida kwenye mpira wa miguu hivyo wachezaji wasife moyo waendelee kupambana.

Related Articles

Back to top button
Bongo5

FREE
VIEW