Habari

Video: Rais Magufuli atoa agizo BOT

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli ameitaka Benki Kuu ya Tanzania(BOT) kusimamia vizuri benki wanazozifungua nchini.

Rais Magufuli ameyasema hayo leo akiwa mjini Dodoma leo wakati akizindua tawi la Benki ya CRDB, ambapo ametoa mfano kuwa kuna nchi ambayo ilionyesha Makao Makuu yake Tanzania lakini fedha ilizokuwa inaweka ni nchi ambazo zina mambo ya ajabu.

“Benki Kuu muanze kusimamia vizuri hizi benki mnazozifungua hapa, mliwahi kufungua benki moja ambayo ilionekana Makao Makuu yake yako Tanzania, lakini fedha zilizowekwa Tanzania ni less than 10 percent zile zingine zilikuwa zinawekwa kwenye nchi ambazo zina mambo ya ajabu ajabu yanafanyika,” amesema Rais Magufuli.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents