Habari

Video: Rais Magufuli atoa neno kwa waandishi wa habari ‘Nyie na sisi tunateseka pamoja’

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt John Pombe Magufuli amewapongeza waadishi wa habari wa Tanzania huku akiwaahidi kuwa atatafuta wakati akae na waandishi wote ili kuzungumzia changamoto zinazowakabili ikiwa ni pamoja namna gani serikali itawasaidia ili wawe Top class.

Rais Magufuli ameyasema hayo alipokuwa akizungumza na waandishi wa mkoa wa Kagera katika ziara yake mkoani humo ambapo amesema kuwa yeye yuko tayari hata kutenga fedha za kwaajili ya mafunzo kwa waandishi wa habari.

“Niwapongeze waandishi wa Kagera kwa kuandika vizuri shughuli za serikali napenda kuwahakikishia kwamba serikali itaendelea kushirikiana na serikali ya Tanzania nawaandishi wa Kagera katika kuwaletea Maendeleo Watanzania hongereni sana tunawapenda endeleeni kutoa ushirikiano huu kwa vyombo vyote hongereni sana waandishi Oyee!,” alisema Rais Magufuli.

“Msiakate tamaa najua mna changamoto nyingi lakini siku moja tutatafuta wakati muafaka tukae na waandishi tuzungumzie changamoto za waandishi ni namna gani serikali inaweza ikafanya kwaajili ya kusaidia waandishi wa Tanzania, tunataka waandishi wa Tanzania wawe Top Class, mimi hata kama nikutenga fedha kiasi fulani kuwasaidia na kuwapa training am ready nataka muwe organised vizuri kama chama chenu kipo cha Waandishi, hata kama nikutoa waandishi fulani fulani katika kila mkoa mpate training serikali yangu ipo tayari, na ninyi ili nataka nilizungumze kwa dhati kwasababu moyo wangu, ninyi na sisi tunateseka pamoja lazima twende pamoja mmeshiriki kikamilifu katika kushiriki kutufanya sisi tuwe viongozi katika nchi hii,aliongeza.

“Siwezi kuwatupa mchango wenu ni mkubwa sana na hili nazungumza kwa dhati ya moyo wangu, nilipiga push up hapa Karagwe msingeitoa ile push up hakuna mtu ambaye angeiona wa Dar es salaam mlifanya kazi hiyo nyinyi waandishi kwahiyo kama ni kampeni mlipiga kampeni ya kutosha.”

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents