Habari

Video: RC Makonda apewa gari, awataka wananchi kufanya maamuzi kuhusu gari hiyo

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda amekabidhiwa gari aina ya Wingle 5 na Kampuni ya Great Wall Motors ya nchini China kwa kushirikiana na kampuni ya wazawa ya Kifaru Motors (T).

Akielezea sababu ya kukabidhi gari hiyo kwa serikali ya Mkoa wa Dar es Salaam Meneja Mwandamizi wa Kampuni hiyo nchini Afrika Kusini Jianguo Liu ameeleza kuwa ni kuunga mkono jitihada za serikali ya awamu ya tano chini ya Rais John Pombe Magufuli.

Meneja Liu ameeleza kuwa gari hiyo inathamani ya shilingi milioni 55, hivyo itumike kutatua changamoto mbalimbali.

Kwa upande wake RC Makonda amewashukuru wahisani hao kwa msaada huo na kuahidi kuutumia msaada huo kama ilivyokusudiwa, huku akieleza kuwa utaratibu wa kulitumia gari hilo utatokana na maoni ya wananchi ambapo watapiga kura kupitia namba maalumu na kueleza gari hilo liende kwenye idara ipi, kwa mfano idara ya elimu, afya, polisi nakadhalika, zoezi hilo litachukua siku kumi.

RC Makonda ameongeza kuwa serikali yake itaendelea na utaratibu huo wa kupigia kura magari yaende kwenye idara ipi ili kuchochea ufanisi wa kazi na wanachi ndiyo watakao kuwa waamuzi wa hilo.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents