Habari

Video: Revolt TV ya Diddy kuanza kwenda hewani rasmi leo (Oct 21)

Hatimaye ‘the biggest network launch in cable history’ ina masaa machache kabla haijatokea, Revolt TV ya rapper na mfanyabiashara Diddy inatarajiwa kuanza kwenda hewani rasmi leo (October 21) kupitia Comcast na Time Warner Cable.

Diddy-Revolt

Forbes hawakukosea kumuweka katika nafasi ya kwanza ya wasanii wa hip hop walioingiza mkwanja zaidi mwaka 2013 ‘Cash Kings’ sababu Diddy anajua sana kufanya kampeni ya biashara zake, amekuwa akiipromote Revolt Tv kwa miezi kadhaa sasa kupitia akaunti zake za Instagram na twitter kama mtu mwenye njaa vile.

Kupitia Instagram jana Diddy ameweka post nyingi za kuwakumbusha watu juu ya uzinduzi wa Revolt Tv na kuandika,

“HISTORY WILL BE MADE TOMORROW…@REVOLTTV GOES LIVE ON AIR ON #COMCAST AND @TimeWarnerCable ..IF YOUR CABLE PROVIDER DOESN’T CARRY IT HIT THEM ON THEIR TWITTER ACCNT AND SAY #NEEDREVOLT. WE ARE GOING TO RAISE THE BAR. THIS IS ARTISTIC EXCELLENCE!!!! #REPOST TO THE WORLD…” Ujumbe huu Diddy alirudia kuupost mara nyingi huku akitumia picha tofauti.

Baadae aliandika,
“Less than 24hrs away!!! @revolttv will be in your homes!! Are you ready for the revolution?!?! Special thanks to @TimeWarnerCable & #Comcast for making this dream come true!! #REVOLT #GETREADY #REPOSTTOTHEWORLD !”

Tazama video ya tangazo la Revolt TV

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents