Bongo Movie

Video: Rose Ndauka aweka wazi alichojifunza kwenye ziara ya Ramsey Nouah

Msanii wa filamu Bongo Rose Ndauka amefunguka alichojifunza kutoka kwa Ramsey Nouah wa Nigeria katika ziara yake aliyoifanya Tanzania siku chache zilizopita.

“Nimepokea vitu vingi kwanza mabadiliko, yaani kama unahitaji mabadiliko yanaanza kwako wewe mwenyewe binafsi. Kwa hiyo nilichogundua kwamba wasanii watanzania vitu ambavyo tunalalamika hapa tatizo nini na wenzetu na wenzetu wanakutana na vitu kama hivyo wanakutana na vitu hivyo hivyo,” Ndauka ameiambia Bongo5.

Muigizaji huyo ameongeza kwa kusema, “Lakini namna gani unataka kupiga hatua kwenda mbee hilo ndio linakuwa suala. Kwangu mimi ujio wa Ramsey Nouah kwa semina ametupatia leo nimejifunza vitu kutoka kwake na nimejifunza kuchukua Confidence yangu asilimia 100 na kuendelea kupambana na vitu vyangu nilivyokuwa navyo.”

Ramsey alikuwa na ziara nchini Tanzania wiki iliyopita na aliweza kutembelea kaburi la Marehemu Steven Kanumba pamoja na kukutana na waigizaji wa filamu nchini.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents