Burudani

Video: Sallam afunguka tuhuma za kumfanyia ‘figisu’ Alikiba kwenye tamasha la Mombasa Rocks

Baada ya Alikiba kudai alifanyiwa ‘figisu’ kwenye tamasha la Mombasa Rocks Music [Festival] lililofanyika weekend iliyopita huku akimtuhumu meneja wa Diamond, Sallam kuhusika, Sallam amefunguka na kuzungumzia tuhuma hizo pamoja na kilichompeleka katika tamasha hilo.

Sallam

Kiba alitumbuiza nyimbo mbili tu kabla ya mic aliyokuwa anaitumia kuonekana kupata mushkeli/kuzimwa na kumlazimu kuondoka jukwaani na muda mchache baadaye akapanda Chris Brown.

Akiongea katika kipindi cha Mambo Mseto cha Radio Citizen ya Kenya na Willy M Tuva, Sallam amekanusha moja kwa moja kuhusika kwenye tukio hilo.

“Pale mimi nilienda kuangalia show na kuja kufanya connection zangu ambazo zinaendelea. Tulikuwa na Wizkid Tanzania alivyotoka kufanya show ya Fiesta tulikuwa naye Dar es Salaam na akakutana na Diamond. Pia meneja ambaye anasimamia kazi za Diamond West Africa ni Mr Sande ambaye ndiye meneja wa WizKid, kwahiyo shughuli zote nyingine ambazo zinafanyika West Africa yeye ndiye anashughulikia hivyo vyote. Kwa hiyo hiyo ndio kazi ambayo imenileta, na uwepo wangu wote nilikuwa na team ya WizKid,” alisema Sallam.

Aliongeza, “Kwahiyo mimi kuja hapa kilikuwa ni kitu cha kawaida kabisa, kwa sababu kulikuwa na mameneja wa wasanii wengine ambao wasanii hao hawakuwa kwenye show, sijui kama Sauti Sol waliperform lakini najua hawakuperform lakini walikuwepo pale pamoja na mameneja wao, wasanii wengi walikuwa na mameneja wao pale. Unaweza kuona ni jinsi gani kulikuwa na opportunity ya kuja pale na kukutana wadau mbalimbali pamoja na kujifunza vitu wanavyofanya wenzetu. Sasa kama unanituhumu mimi kuwepo pale, usinichukie mimi kwa sababu mimi nakuwa na access, kama kuna kitu unahitaji kwangu nifuate usiogope, kwa sababu sisi wote ni watanzania. Pia wakati anaperform mimi sikuwepo kabisa pale, na hicho kitu media zote ziliona kwa sababu kamera nyingi zilikuwa kwangu, na wakati anafanya show AliKiba mimi niliwa mbali kabisa.”

Akielezea kilichotokea mpaka AliKiba akazimiwa Mic, Sallam alisema “Alifanya show Vanessa Mdee baada ya Vanessa Mdee alitakiwa Ali apande, kwa dakika 30 show ilisimama wakimngoja Alikiba, Alikiba hataki kufanya show mpaka Wizkid afanye show halafu yeye ndo afanye, sawa mimi sijui hizo habari ambazo zinasikika Alikiba ni mkubwa kuliko Wizkid, baada ya dakika kadhaa nikamuona Sande anasema acha tuwape dakika 10 kama asipopanda sisi tutampandisha msanii wetu.

Baada ya hapo Mr Sande akamwambia stage meneja lets go with WizKid, Sande akamchukua msanii wake na kumpandisha kwenye stage. Ndipo na mimi nikapanda kwenye stage kwa sababu nilikuwa na access nilikuwa nao, baada ya kumaliza WizKid tulishuka wote, niliiona team ya AliKiba wakati wanaswali pale chini, kwahiyo wale walikuwa wanapanda sisi tunashuka, kwahiyo mimi niliondoka kabisa kwenye stage.”

“WizKid alipanda kwenye gari na Dj Maphorisa, mimi na Sande tuliingia kwenye room, na muda huo sisi tulikuwa mita 50 kutoka kwenye stage hatuelewi nini kinatokea. Kitu ambacho mimi nilisikia kule kulikuwa na ugomvi mwingine, security wa Chris Brown na stage meneja wanagombana kutaka AliKiba ashuke, kwa sababu ratiba yao Chris Brown anatakiwa show yake iishe saa saba. Chris alishasema anataka kuperform saa 5 kamili awe kwenye stage, kwa hiyo tayari walikuwa wameshachelewa, kwahiyo kitu kingine ambacho nilisikia muziki umezimwa, Chris anaenda kufanya show, akapigiwa simu Sande na WizKid njoeni hapa, tukaenda.”

Kwa upande mwingine Sallam amesema Ali anapaswa kuwaomba msamaha mashabiki kwa kilichotokea na kumbebesha mzigo yeye kwa kitu ambacho hakuhusika nacho. Anadai kwa alichokisema, ameonesha dhahiri kuwa ana chuki na Diamond.

“Nataka nimwambie Alikiba najua atasikisikia hii kitu, ‘Alikiba, next wikiendo tutakuwepo MTV and I will be at the backstage again so don’t be scared. Afanye kazi vizuri , aje kwenye stage tulipresent East Africa vizuri, asipaniki, mimi ni mtu wa kawaida na akiniona anisalimie wala asiniogope. Kitu ambacho amekionesha, ameonesha dhahiri chuki ya Diamond,” amesisitiza.

“Sababu Diamond ni mtu ambaye alikuwepo Tanzania wala hahusiki.”

Sallam amemuomba Alikiba kuacha kuongea vitu ili kuwafanya Wakenya wamchukie Diamond.

“Wakenya wanatakiwa waombwe msamaha kwa kitu ambacho amekifanya na kitu ambacho amewadanganya Jumuiya yote ya East Africa. Mimi asiponiomba msamaha sawa, mimi nishamsamehe na naomba apunguze chuki kwa Diamond ili tuendelee, tufanye muziki kwa pamoja, Diamond hahusiki kabisa na mambo yake.”

Meneja huyo amesisitiza kuwepo upendo kwenye muziki wa Afrika Mashariki na kwamba chuki haijengi.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents