Burudani

Video: Salma wa BSS 2013 aungana na Mi Casa Cassper Nyovest, Donald, Oliver Mtukudzi kwenye Coke Studio SA

Aliyewahi kuwa mshindi wa pili kwenye mashindano ya Bongo Star Search mwaka 2013, Salma Yusuf ameungana na mastaa wa Afrika Kusini kwenye msimu mpya na wa kwanza wa Coke Studio South Africa.

salma 3
Salma Yusuf (wa pili kutoka kulia) aliwahi kuwa muimbaji wa Skylight Band

Show ya kwanza ilioneshwa wiki iliyopita na kuwashirikisha wasanii wakubwa wakiwemo Mi Casa na Cassper Nyovest.

Coke Studio South Africa inatofautiana na Coke Studio Africa inayofanyika jijini Nairobi, Kenya.

Pamoja na Salma, wasanii wengine wanaoshiriki kwenye kipindi hicho ni pamoja na Donald, Goodluck, Uhuru, Oliver Mtukudzi na Black Motion.

salma 2

Salma ni msanii pekee kutoka Afrika Mashariki anayeshiriki kwenye show hiyo.

Watu wengi wamependa uwezo wa Salma ambapo mtu mmoja amepost video ya Salma na kuandika: So excited about tonight’s #CokeStudioZA episode on ETV at 8:30. Salma has such a haunting and beautiful voice. She sings in Swahili here.”

sala

Baada ya kutoka BSS Salma alijiunga na bendi ya Skylight kabla ya kuhamia nchini Afrika Kusini.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents