Videos

Video: Samaki Samaki tawi la Mbezi, Dar iliungua kutokana na moto uliotokana na cheche za greda

Uongozi wa msululu wa migahawa ya Samaki Samaki ya jijini Dar es Salaam, leo umefanya mkutano na waandishi wa habari kueleza chanzo cha ajali ya moto iliyotokea asubuhi siku ya Jumanne, August 27 na kuliteketeza tawi lake la Mbezi Beach, Makonde.

Akitoa taarifa hiyo, Afisa Maendeleo wa Samaki Samaki, Ng’winula Kingamkono amesema ajali hiyo ilitokea wakati ubomoaji ili kupisha ujenzi wa bomba la maji ukiendelea. Amesema wakati gari la kubomoa lilipoanza kazi ndipo moto huo ulipozuka.

“Moto huo ambao ulisababishwa na cheche zilizotokana na greda iliyokuwa ikiendelea na tukio la ubomoaji wa jingo la tawi letu la Mbezi beach, uliteketeza samani na mali zote zilizokuwepo (thamani haijulikani) bila kusalia chochote,” alieleza Kingamkono.

“Hakuna yeyote aliyekufa wala kujeruhiwa katika janga hili,” aliongeza.

“Tumepata hasara kubwa na hatujui thamani kamili ya vifaa vilivyoteketea ila uchunguzi unaendelea kwenye vyombo husika,”alisema.

Pia aliongeza kuwa kutokana na kuungua kwa tawi hilo la Mbezi beach, kwa sasa wapo kwenye utaratibu wa kufungua lingine maeneo ya Masaki jijini Dar es Salaam.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents