Michezo

Video: Samatta aiokoa Genk kutoka kwenye kipigo ligi kuu

Mshambuliaji wa KRC Genk na Taifa Stars, Mbwana Samatta usiku wa jana amefanikiwa kuikoa timu yake kutoka kwenye kipigo kwenye ligi kuu ya Ubelgiji.

Samatta lifanikiwa kufunga bao moja katika sare waliyoipata ya kufungana bao 1-1 dhidi ya KAA Gent.

Gent walikuwa wa kwanza kupata bao lao kupitia kwa Yuya Kubo dakika ya 15, Hata hivyo Samatta alisawazisha bao hilo katika dakika ya 66.

Kwa sasa KRC Genk inashika nafasi ya sita katika ligi kuu nchini humo wakiwa na jumla ya alama 32 wakati Club Brugge wakiongoza ligi hiyo wakiwa na alama 45.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents