Michezo

Video: Samatta atupia akitokea benchi, KRC Genk ikichomoza na ushindi dhidi ya W. Beveren

Mshambuliaji hatari zaidi ndani ya klabu ya KRC Genk ya Ubelgiji raia wa Tanzania, Mbwana Samatta hapo jana ameisaidia timu yake kuchomoza na ushindi wa jumla ya mabao 3 – 2 dhidi ya W.Beveren kwa kuipatia bao akitokea benchi mchezo wa ligi kuu nchini Ubelgiji (First Division).

Wachezaji wa KRC Genk walipata bao la mapema kupitia kwa Edson Zhegrova dakika ya 20, Mbwana Samatta dakika ya 78 na Maximiliano Caufriez dakika ya 89 wakati ya W. Beveren yakifungwa na Nana Opoku Ampomaha dakika ya 66 na 75.

Matokeo hayo yameifanya klabu ya KRC Genk kuongoza kwenye msimamo wa ligi kuu Ubelgiji kwa kuwa na jumla ya ponti 13 ikikimbizwa kwa karibu zaidi na Club Brugge.

Related Articles

6 Comments

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents