Diamond PlatnumzVideos

Video: Sebastian Maganga azungumzia umuhimu wa wasanii kuthubutu waonapo fursa ya kukubalika

Mtangazaji mkongwe wa radio nchini, Sebastian Maganga ambaye kwa sasa ni meneja wa vipindi wa Clouds FM, amesema wasanii wanapaswa kuwa na moyo wa kuthubutu pale wanapoona fursa za kukubalika.

Akimtolea mfano Diamond Platnumz, Seba aliyewahi kuwa mtangazaji wa Radio One na Radio Uhuru, amesema wasanii wa Tanzania wanatakiwa kuwekeza katika kila hatua ili kwenda juu zaidi.

“Diamond tangu alivyopewa fursa kwa mara ya kwanza katika Serengeti Fiesta miaka kama minne iliyopita alithubutu na akaexceed yale matarajio ya kawaida,” alisema Seba aliyekuwa kwenye uzinduzi wa video mpya na wimbo wa Diamond, Number 1.

“Watu wakahisi labda ni kitu cha hapo kwa hapo, wakahisi kwamba pengine hiyo ni kwaajili ya jukwaa tu ataishia hapo, lakini toka pale mpaka leo hii amezidi kututhibishia kwamba, vision yake aliyokuwa nayo, sio vision ya kitoto ni vision kubwa ajabu. Kwahiyo tunahitaji watu kama hao ambao wana vision kubwa na wengine ambao wana uwezo mkubwa waweze kushirikiana, waweze kutupeleka mbele.”

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents