Habari

Video: Serikali inaheshimu Muhimili wa Bunge – Waziri Mkuu

Leo Bungeni kuna kuwa na maswali ya PAPO KWA PAPO kwa Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa ambapo waziri Mkuu anajibu maswali mbalimbali kwa wabunge. Katika nafasi ya Wabunge waliopata nafasi ya kuuliza swali alikuwa ni Kiongozi wa Kambi ya upinzani Bungeni, Freeman Mbowe.

Baada ya kupewa nafasi ya kwanza kumuuliza swali Waziri Mkuu, Mheshimiwa Mbowe aliulizwa swali hili:

“Muheshimiwa Waziri Mkuu Bunge kwa mujibu wa Katiba katika Ibara ya 63 fasili ya 2 ndicho chombo kikuu chenye mamlaka na wajibu wa kuisimamia na kuishauri Serikali na katika bunge hili katika Bunge la 10 na Mabunge mengine kadhaa, Bunge limekuwa linatoa maazimio kadhaa kuitaka serikali itoe taarifa na serikali imekuwa ikiahidi kutoa lakini taarifa nyingi ambayo ni maazimio ya Bunge yamekuwa hayatekelezwi na Serikali,huku akitoa mfano suala la ESCROW, Muheshimiwa Waziri Unaliambia nini Bunge na unaliambia nini Taifa,wewe kama kiongozi wa serikali Bungeni, utapenda kusema serikali inalidharau Bunge au serikali haina majibu ya kutoa? alihoji Mhe. Mbowe

Waziri Mkuu akijibu swali hilo amesema,”Kwanza naomba nikuhakikishie kwamba Serikali ina heshimu sana Muhimili wa Bunge, na inaheshimu sana maamuzi ya muhimili huu na tutaendelea kushirikiana na muhimili wa Bunge katika kupata ushauri na namna ya kuendesha serikali lakini, pamojja na mapendekezo yanayotolewa na waheshimiwa Wabunge kupitia chombo cha Bunge,natambua vikao vya hapo awali na huko nyuma kumekuwa na maazimio yanayotaka serikali ilete maelezo lakini baadhi ya maeneo yanayotakiwa kuletwa hapa ni yale ambayo yanahitaji uchunguzi wa Kina na uchunguzi huo unapofanyika unatakiwa kuletwa hapa Bungeni.”

Video: Majibu ya Serikali

Na Emmy Mwaipopo

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents