Habari

Video: Serikali kuanzisha bima ya kukosa ajira

Waziri wa Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Walemavu, Jenista Mhagama amesema Serikali pamoja na wafanyakazi wamekubaliana kuangalia namna nzuri ya kuwasaidia wafanyakazi wote ambao wamekuwa wakikumbwa na suala la Mafao kwa kuanzisha fao jingine ambalo litaitwa Bima ya kukosa ajira.

Waziri Muhagama alitoa kauli hiyo Bungeni, Mjini Dodoma wakati akijibu swali la mbunge Innocent Bashungwa lililohoji

Kumekuwa na changamoto kubwa ya vijana wanaoajiliwa kwa mkataba wa muda mfupi kuzungushwa pale wanapotaka mifuko ya pensheni kudai mafao yao ili waweze kuitumia kama mitaji ya kujiajiri

Waziri Muhagama alisema “Kupitia sera ya hifadhi ya jamii katika nchi yetu, serikali pamoja na wafanyakazi wenyewe na vyama vya wafanyakazi tumekubaliana sasa kuna haja ya kuangalia namna nzuri ya kuwasaidia wafanyakazi wote ambao wamekuwa wakikumbwa na jambo hilo kwa kuanzisha fao jingine ambalo litaitwa ‘Bima ya kukosa ajira‘ ,” alisema Muhagama.

“Mheshimiwa Naibu spika kazi hiyo tumeshaanza kwa kushirikiana na vyama vya wafanyakazi kwa hiyo niwaombe wafanyakazi wote nchini ambao walikuwa wanaelekea katika fao hilo wavute subira ili matakwa ya kisheria yafanyiwe kazi na ndipo fao hilo litaanza kutolewa kwa mujibu wa sheria ambayo itakuwa imetungwa na bunge na pia maagizo ya Mheshimiwa Rais siku ya Mei Mosi alipokuwa pale Moshi ameendelea kusisitiza kwa sasa tushughulikie suala hilo na liweze kufungwa kisheria na wafanyakazi waweze kupata haki zao.”

Video: Haya ni Majibu ya Serikali

Na Emmy Mwaipopo

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents