Habari

Video: Serikali kuanzisha zoezi la uandikishaji mifugo

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa amesema kuwa serikali ina mpango wa kuanzisha zoezi la kuandikisha mifugo ili waweze kutambua ni kijiji gani, kina nani na ana mifugo kiasi gani ili iweze kutambua kama mifugo iliyopo eneo hilo inatosha kukaa eneo hilo.


Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa

Hayo yamezungumzwa na Waziri Majaliwa akiwa bungeni mjini Dodoma wakati akijibu swali mbunge Zuberi Kuchauka lililohoji,

Tanzania ni nchi ambayo ina mifugo mingi sana na wafugaji wetu wengi ni wafugaji wa kuhamahama,Jambo hili limetuletea migogoro sana ya ardhi mpaka kusababisha mauaji, Lakini sasa kumezuka mtindo mikoa ile ya wafugaji tayari watu wanahama kwenda mikoa ambayo sio yawafugaji kwa asili na maana nini migorogoro ya mauaji haya ya wakulima na wafugaji tunaihamishia kwenye hii mikoa ambayo si ya wafugaji, nini kauli ya serikali juu ya kusambaza haya mauaji ya wakulima na wafugaji katika mikoa ambayo si ya wafugaji?

“Jambo hili serikali tumekuwa tukifanya namna nzuri ya kundi hili la wafugaji na mifugo yao lakini pia wakulima waendelee na shughuli zao za kilimo kwa kuanza zoezi la uandikishaji wa mifugo tuweze kuitambua ni kijiji gani kina nani ana mifugo kiasi gani na mifugo ya kiasi gani ili tuweze kuona kama je mifugo hiyo inatosha kukaa. Hivi leo nimeita Maafisa mifugo wa nchi nzima wako hapa saa tano nakutana nao pale chuo cha Mipango yapo maeneo ambayo waheshimiwa wabunge wakulima na wafugaji watuvumilie, serikali tuchukue mkondo wetu,” alisema Majaliwa.

“Tunahitaji sasa tuanze kujua utaratibu mzuri wa ufugaji kwasababu tunataka tuwapate wafugaji ambao kweli ni wafugaji wanaofuga ambao wako serious kwenye ufugaji, lakini ufugaji huu lazima uendane na maeneo ya kulisha ili tuondokene na migogoro ya wakulima na wafugaji yanayopelekea mauaji ambayo mheshimiwa mbunge ameongea.”

Video:

Na Emmy Mwaipopo

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents