Habari

Video: Serikali ya India kutoa shilingi dola milioni 500 nchini

Serikali kupitia Wizara ya Maji na Umwagiliaji imesema kuwa Serikali ya India imeahidi kutoa dola milioni 500 kwa ajili utekelezaji wa miradi ya maji katika miji 16 ya Tanzania Bara na Zanzibar katika mwaka wa fedha 2017/18.


Naibu Waziri wa Maji na Umwagiliaji Mhe.Eng.Isack Kamwelwe

Hayo yamesemwa na Naibu Waziri wa Maji na Umwagiliaji Mhe.Eng.Isack Kamwelwe akijibu Swali la Mbunge wa Tumbatu Mhe.Juma Othman Hija leo Bungeni Mjini Dodoma lililohoji

wakati wa hotuba ya Bajeti mwaka 2016/2017 wizara ya maji na umwagiliaji ilionyesha kuwa serikali ya india imesaidia kiasi kikubwa cha fedha kwaajili ya maji je Serikali inaweza kutueleza utekelezaji wa jambo hilo?

“Katika bajeti ya mwaka 2016/17 Wizara yangu ilitoa taarifa ya mchango mkubwa inaoupata kutoka Serikali ya India ili kuboresha huduma ya Maji nchini kwakupitia mkopo wa masharti nafuu kutoka Serikali ya India awamu ya kwanza serikali ya Tanzania ilipata dola za Kimarekani Milioni 178.125,” aliongeza Mhe.Kamwelwe.

Aidha katika awamu ya tatu hatua inayoendelea kwa sasa ni kufanya manunuzi ya Mhandisi Mshauri atayefanya mapitio ya usanifu wa miradi na uandaaji wa makabrasha ya zabuni kwa ajili ya ujenzi ambapo kazi ya ujenzi zinatarajiwa kuanza katika mwaka wa fedha 2017/18.

“Katika awamu ya Pili Serikali ya India itatoa dola milioni 268.35 kwa ajili ya mradi mkubwa wa kutoa maji katika mradi wa KASHWASA kutoka kijiji cha Solwa kwenda katika miji ya Tabora,Igunga,Nzega,Tinde na Uyui pamoja na Vijiji 89 vinavyopitiwa na bomba kuu umbali wa kilomita 12 kila upande uku wakandarasi wa kutekeleza mradi huo wamepatikana na wapo katika hatua ya maandalizi ya utekelezaji za utekelezaji.

“Katika awamu ya tatu Serikali ya India imeahidi kutoa fedha kiasi cha dola Milioni 500 kwaajili ya utekelezaji wa maji katika miji 16 ya Tanzania Bara pamoja na miradi ya maji kwa upande wa Zanzibar,” alieleza.

Video: Wizara ya maji

Na Emmy Mwaipopo

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents