Habari

Video: Serikali yaeleza ilivyofaidika mkataba wa sekta ya afya na Cuba

Naibu Waziri wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Ustawi wa Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto amesema Serikali Tanzania imepokea madaktari bingwa kutoka Cuba, ambao wamekuwa wakitoa huduma mbalimbali za kibingwa katika hospitali ya Muhimbili, hopsitali ya Rufaa ya Mbeya,Tumbi na hospitali ya Rufaa ya mkoa wa Ruvuma.

Dkt Kigwangalla ameyasema hayo leo Bungeni wakati akijibu swali la Mbunge wa Gando, Othumani Omari Haji lililohoji

Je, ni kiasi gani Tanzania imefaidika na mkataba iliyoingia na nchi ya Cuba kuhusu uboreshaji huduma za afya nchini?

“Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, imekuwa ikishirikiana na serikali ya Cuba katika mambo mbalimbali ikiwa ni pamoja na sekta ya Afya tangu 1986 ambapo mkataba ulisainiwa kati ya serikali hizi mbili. Kupitia mkataba huo Serikali ya Tanzania imekuwa ikipokea madaktari bingwa kutoka Cuba, ambao wamekuwa wakifanya kazi katika hospitali za Muhimbili, hospitali ya Rufaa ya kanda ya Mbeya, Hospitali ya Tumbi na Hospitali ya Rufaa ya mkoa wa Ruvuma, Madaktari hawa wamekuwa wakitoa huduma mbalimbali za kibingwa kwa wananchi na kuwajengea uwezo madaktari wanaofanya nao kazi katika hopsitali hizo,” amesema Naibu Kigwangalla.

Video: Dkt Kigwangalla anatoa majibu ya Serikali:

Na Emmy Mwaipopo

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents