Habari

Video: Serikali yafafanua ongezeko la wagonjwa wa Kisukari nchini

Waziri Ummy ameyazungumza hayo Bungeni mjini Dodoma wakati akijibu hoja mbalimbali za wabunge amekiri kushuhudia ongezeko la watu wenye kisukari.

“Ni kweli tunashuhudia ongezeko la Kisukari, lakini kwasababu kwanza ya mfumo wa maisha ambao watu wanaishi watu hawafanyi mazoezi, wanakula vyakula bila kuzingatia lishe lakini pia bila kucheki afya zao mara kwa mara, kwahiyo badala ya kujikita kwenye kutibu tumejikita kwenye kuzuia Watanzania wengi wasipate maradhi ya ugonjwa wa kisukari,” alisema waziri Ummy.

“Lakini pale ambapo Mtanzania ana ugonjwa wa Kisukari kwa mujibu wa sera ya afya,dawa ya mgonjwa wa kisukari inatakiwa kupatikana kwa bei nafuu kwahiyo tuwaelekeze tunawaelekeza waganga wakuu wa wilaya na mikoa wanapoandaa maoteo ya dawa basi wahakikishee wanaoda dawa za kisukari kama hawawezi kuoda hatuwezi sisi kuwapelekea.”

Video: Tazama majibu ya serikali

Na Emmy Mwaipopo

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents