Habari

Video: Serikali yatoa utaratibu wa kuhamisha na kuwapangia kazi watumishi wa umma

Serikali kupitia wizara ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma,imesema kuwa Utaratibu wa ajira ufanyika kwa mujibu wa sheria ya utumishi wa umma namba 8 ya mwaka 2002, ambapo mchakato wa ajira hufanywa na sekretarieti ya utumishi wa umma ambayo hutangaza kazi kulingana na mahitaji ya waajiri.

Hayo yamezungumzwa leo bungeni mjini Dodoma na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Angella Kairuki ambaye amesema Kazi ya ualimu na ile ya afya, utaratibu wao wa kuajiriwa ni mara baada ya wanapohitimu mafunzo yao.

“Ukiacha watumishi wa Kada ya ualimu na wale wa kada za afya, ambao utaratibu wao wa kuajiriwa ni mara baada ya wanapohitimu mafunzo yao. Utaratibu wa ajira kwa kada nyingine ufanyika kwa mujibu wa sheria ya utumishi wa umma namba 8 ya mwaka 2002, kwa mujibu wa sheria hii mchakato wa ajira hufanywa na sekretarieti ya utumishi wa umma ambayo hutangaza kazi kulingana na mahitaji ya waajiri kufanya usahili wa kuwapeleka katika vituo vya kazi wombaji walio faulu usahili,” amesema Kairuki.

“Uhamisho ndani ya utumishi wa umma hufanywa kwa mujibu wa sheria ya utumishi wa umma sura ya 298 inasema kwa pamoja na kanuni za kudumu za utumishi wa umma za 2009 ambapo Katibu Mkuu Utumishi amepewa mamlaka ya kuhamisha watumishi wa umma kutoka kwa muajiri mmoja kwenda muajiri mwingine kwa lengo la kuhamasisha utendaji ndani ya utumishi wa umma, vigezo vinavyotumika kuwapanga na kuwahamisha vituo vya kazi watumishi wa umma ni pamoja na moja ya mahitaji ya kila taasisi kutokana kuwepo kwa ukame bajeti ya mshahara kwa watumishi kwa mwaka wa fedha husika mbili kutokan na sifa za kitaalumu, umuhimu wa kuimarisha utendaji wa kazi,” amefafanua Kairuki

Swali lilihoji hivi

“Ni utaratibu upi serikali hutumia kuhamisha na kuwapangia kazi watumishi wa umma?

Swali hilo liliulizwa na Mh.Riziki Shahari Mngwali Mbunge wa Viti Maalum.

Video: Waziri Angella Kairuki anatoa majibu ya Serikali

Na Emmy Mwaipopo

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents