Habari

Video: Serikali yaweka wazi haki za wafungwa nchini

Waziri wa Mambo ya ndani ya nchi, Mwigulu Nchemba amesema wafungwa hutenganishwa kutokana na umri wao, jinsia, aina ya kosa, afya pamoja na tabia huku akisema wana haki za kupata mawasiliano kutembelewa na ndugu na majamaaa zake, mawasiliano haya ni pamoja na kusikiliza magazeti, kusikiliza taarifa mbalimbali.

Waziri Nchemba ameyasema hayo mjini Dodoma wakati akijibu swali la Zubeda Hassan Sakulu mbunge wa viti maalumu aliyetaka kujua haki za wafungwa Magerezani.

“Jeshi la Magereza limekuwa likitekeleza na kusimamia haki za wfungwa Magerezani kwa kuzingatia sheria namba 34 ya mwaka 1967 pamoja na sheria zingine na kanuni za uendeshaji magereza. Aidha haki za wafungwa zinazotekelezwa na kusimamiwa Magerezani kwa mujibu wa sheria ya Magereza na kanuni zake nilizozitaja au misingi mingine chimbuko lake ni mikataba ya kimataifa zinazohusu haki za wafungwa na Mahabusu,” alisema Mwigulu.

“Wafungwa hutenganishwa kutokana na umri wao, jinsia, aina ya kosa, afya pamoja na tabia, lakini ya pili ni haki ya kupewa chakula na mahitaji mengine, mfungwa hupewa chakula kama ilivyohainishwa kama ilivyoanishwa na kanuni ya uendeshaji wa Magereza niliyo itaja, haki ya kuwa na uhuru wa kupata mawasiliano kutembelewa na ndugu na majamaaa zake, mawasiliano haya ni pamoja na kusikiliza magazeti, kusikiliza taarifa mbalimbali kutoka kwenye vyombo vya habari na nyingine ni pamoja na huduma za afya huduma hizi hutolewa kwa mfungwa pindi anapokuwa anaumwa wakati wowote awapo gerezani.”

Video: Tazama Waziri Mwigulu Nchemba akitoa majibu ya Serikali

Na Emmy Mwaipopo

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents