Habari

Video: Shaa asitisha kuiachia video yake mpya ya wimbo Sawa, apata hasara ya tsh milioni 60

Msanii wa muziki Shaa amesitisha kuiachia video yake mpya ya wimbo ‘Sawa’ kutokana na video hiyo kutoendana na matendo ya wimbo huyo.

Video hiyo ambayo alishoot na director Justin Campos wa Afrika Kusini, ilimgharimu dola 30,000 sawa na zaidi ya tsh milioni 60 za Tanzania.

Akiongea na Bongo5 wiki hii, Shaa amedai video hiyo ilikuwa tayari kutoka lakini baada ya kuwaonyesha baadhi ya watu wakamshauri video hiyo asiitoe.

“Mimi napenda kusikiliza ushauri wa watu wangu ambao nimekuwa nikifanya nao kazi kwa muda mrefu. Kwahiyo video tumesitisha kuitoa kwa sababu script haiendani na wimbo,” alisema Shaa.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents