Bongo5 ExclusivesBurudaniDiamond PlatnumzMahojiano

Video: Shetta kuachia ngoma nyingine aliyomshirikisha Diamond Platnumz

Baada ya kufavya vizuri na ‘Nidanganye’ aliyomshirikisha Diamond Platnumz, Shettah amesema ataachia ngoma nyingine tena aliyomshirikisha hitmaker huyo wa ‘My Number One’.

Shetta ameiambia Bongo5 kuwa wimbo huo utatoka mwishoni mwa mwezi huu. “Nina ngoma mpya na Diamond nimefanya naye,”amesema rapper huyo.

Akielezea sababu za kuachia wimbo mwingine na Diamond, Shetta amesema:

Kuimba ni mzuka, nakumbuka tulikuwa kwenye show fulani Tabora nilikuwa na Diamond, nikawa namuimbia verse za hiyo nyimbo yangu akaniambia ‘man hizo verse mbona kama kali hivi’ nikamwambia ‘yeah man, that’s whatsup hicho ndicho kitu nataka kirudi tena’ akaniambia ‘kali sana’ nikamwambia ‘unaweza kufanya kitu?’ akaniambia ofcourse mimi nashindwaje kufanya kitu.”

Shetta amesema wimbo huo umeteyarishwa na producer wa ‘My Number One’ Sheddy Clever.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents