Burudani

Video: Shilole ampa ‘zawadi’ shabiki wa kiume ambayo hatoisahau kamwe – Serengeti Fiesta Dodoma

Kulishika kama utakavyo umbo la kuvutia la mwanadada Shilole ni ndoto ya wanaume wengi. Lakini vipi kama ndoto hiyo ikikuijia katika wakati ambapo hujajiandaa kabisa? Utaona aibu kuitimiza? Huenda jibu hili anaweza kuwa nalo kijana wa Dodoma aliyepata bahati hiyo ya mtende kwenye jukwaa la Serengeti Fiesta mjini Dodoma jana usiku.

Akiwa amevalia nguo iliyolichora vema umbo lake, Shilole alimpa nafasi kijana huyo kuiota ndoto hiyo walau mara moja katika maisha yake. Kijana huyo aliyekuwa amevalia t-shirt nyekundu hakufanya ajizi. Akionesha kufurahia ‘fursa’ hiyo ya aina yake, jamaa alionekana kunogewa kulishika na kulikumbatia umbo la Shilole ambaye alimruhusu afanye chochote.
Chochote lakini sio vyote!!!

Mbele ya umati mkubwa wa wakazi wa Dodoma, Shilole alimruhusu jamaa huyo alikamate kiume paja lake jeupe huku akikata kiuno na kumshika begani.

Tukio hilo lilivuta hisia za maelfu ya wakazi wa Dodoma waliokuwa wakishangalia mwanzo mwisho. Ama hakika, Shilole anajua kuwapa raha mashabiki wake.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents