Habari

Video: Si kweli wanawake wa Kiislam huvuliwa Hijab na Nikab – Serikali

Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya nchi, Hamadi Masauni amesema kuwa Si kweli kuwa wanawake wa Kiislam wanapovaa Hijab au Nikab huvuliwa na maafisa wanaume wa Jeshi la polisi.

Mheshimiwa Masauni ameyazungumza hayo leo bungeni, mjini Dodoma wakati akijibu swali lililoulizwa na mbunge Halima Ally Mohamed, Mbunge wa Viti Maalum lililouliza:

Kwa mujibu wa Ibara ya 19(1) ya katika ya nchi kila mtu ana haki na uhuru wa kuamini dini aitakayo, Je?, Ni kwanini wanawake wa Kiislam wanapovaa Hijab wanavuliwa na maafisa usalama wa kiume?

“Si kweli kuwa wanawake wa Kiislamu wanapo vaa hijab ama nikab wanavuliwa na Maafisa wanaume wa Jeshi la Polisi , Aidha Jeshi la polisi linafanya kazi kwa kuzingazia sheria kanuni na taratibu ya kuliongoza jeshi hilo kwa muhibu wa PGO 103(1) ambayo inasema malalamiko yote zidi ya polisi yatolewe mara moja katika kituo chochote cha eneo na hatua za uchunguzi zifanyike kwa ukamilifu,” amesema Masauni.

“Nawaomba niwaombe wananchi hususani wanawake pindi wanavyofanyiwa vitendo kama hivyo kupeleka malalamiko yao Polisi au kwenye mamlaka nyingine husika ili sheria iweze kuchukua mkondo wake.”

Tazama majibu ya serikali wakifafanua juu ya vazi hilo:

Na Emmy Mwaipopo

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents