Habari

Video: Sijawahi kununuliwa na sinunuliki – Mh. Kubenea

Mbunge wa Ubungo kwa tiketi ya Chadema, Saed Kubenea amesema kuwa hajawahi kununuliwa na huwa hanunuliki.

Kubenea ameyasema hayo Leo, wakati akizungumza na waandishi wa habari huku akieleza kuwa akiamua kufanya jambo lolote lile analifanya kutoka kwenye moyo wake.

“Mimi sijawahi kununuliwa na huwa sinunuliki nikifanya jambo lolote lile nalifanya kutoka ndani ya moyo wangu, kama vishawishi vya fedha nimevipitia vingi sana,” Kubenea.

Aidha Kubenea amesema kuwa “Na pia nimesikia aliyekuwa Mbunge wa Jimbo la Kinondoni Maulid Mtulia nae inasemekana amenunuliwa biashara imefanyika.”

Kubenea ameyasema hayo baada ya taarifa kuenea kuwa na yeye ni mmoja wa watu wanaotaka kuhama Chadema na kuhamia CCM.

 

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents